November 1, 2020

MEELEZWA kuwa Klabu ya Simba imewaondoa wapishi wao wawili ambao walikuwa wakihusika katika kuwapikia chakula wachezaji wa timu hiyo.

 

Hivi karibuni Simba imewashtua mashabiki wao kufuatia matokeo ya kufungwa mechi mbili mfululizo kwenye ligi, ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Prisons kule Nelson Mandela, Sumbawanga kisha iliporejea Uwanja wa Uhuru jijini Dar ikapigwa bao 1-0 na Ruvu Shooting.

 

Awali Simba ilitangaza kuachana na kocha wa makipa Muharami Mohammed na meneja Patrick  Rweyemamu. 

 

Aidha taarifa zingine zinasema kuwa imewapiga chini Ally Shantra na Jacob ambao walikuwa kwenye kitengo cha habari.Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, timu hiyo imefi kia hatua ya kuwafuta kazi wapishi wawili kutokana na hofu ya hujuma kufanyika kwa wachezaji wao. 

 

 

Inadaiwa kuwa, Simba imeamua kuachana nao fasta na kusaka wengine ambao wanawaamini katika utendaji kazi wao kwa kuhakikisha wanawapikia chakula safi  wachezaji na benchi lao la ufundi.

 

“Simba imeachana na wapishi wao wawili kwa hofu ya hujuma kwenye ishu ya vyakula vya wachezaji, wamefanya hivi ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda safi  kwa wachezaji na timu nzima kwa ujumla,” kilisema chanzo hicho.

12 COMMENTS:

  1. Safisha wote wenye connection na Senzo, tunataka Simba ya wenye Simba

    ReplyDelete
  2. Noma sana Hii kumbe kuna watu ndani ya Simba wana mambo yao ya Siri Khaaaah

    ReplyDelete
  3. Fukuza wote wapishi benchi la ufundi tunataka timu ikae sawa inshaallah

    ReplyDelete
  4. Na bado mtafukuzana sana mwaka huu na bado klabu bingwa inawasubiri

    ReplyDelete
  5. ha ha ha ha,kwani wapishi ndio walicheza au ndo mnaweweseka na kipigo tar 7

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani uto mlinfukuza kocha aliwakosea nini?


      HATIMAYE siri imefi chuka kuwa kompyuta mpakato ‘laptop’ aliyokuwa akiitumia mtendaji mmoja wa Simba ndiyo imeonyesha kuwa timu hiyo inahujumiwa na wapinzani wao.


      Hivi karibuni Klabu ya Simba iliwatimua watendaji wake wanne, lakini haikuweka wazi sababu rasmi zilizochangia kuwatimua watu hao.


      Simba iliwatimua Meneja Patrick Rweyemamu, Kocha wa Makipa Muharami Mohammed, Ally Shantra na Jacob ambao wapo kitengo cha habari.


      Timu hiyo imefanya hivyo baada ya kutoka kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye ligi hali iliyozua sintofahamu licha ya kuwa ilifanya usajili mkali kwenye dirisha kubwa lililofungwa Agosti 31, mwaka huu.

      Awali, Simba ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Prisons kule Sumbawanga katika Uwanja wa Nelson Mandela kisha ikapokea kichapo kama hicho dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.


      Chnzo cha ndani kutoka Simba kimelieleza Championi Jumamosi kuwa, hujuma hizi zilibainika baada ya mtendaji mmoja aliyeondolewa kwenye timu hiyo kukabidhi kompyuta ya ofi si ambayo alikuwa anaitumia ilikuwa na meseji kadhaa za mtandao wa WhatsApp kuonyesha kuwa alikuwa na mawasiliano na kigogo mmoja wa timu pinzani.


      “Unajua mara nyingi ukitumia WhatsApp kwenye kompyuta lazima uwe makini sana vinginevyo inaweza kukuumbua.

      “Kuna ofi sa mmoja aliondolewa hapa, lakini kwa kuwa alikuwa anatumia kompyuta ya ofi si alitakiwa kuikabidhi na kwa bahati alikuwa hajafunga WhatsApp yake kwenye kompyuta na hivyo meseji zikawa zinaendelea kuingia zikionyesha jinsi ambavyo amekuwa akiwasiliana na kigogo mmoja mkubwa wa wapinzani.



      “Meseji zile zilikuwa zinaonyesha jinsi ambavyo kigogo huyo anataka kufahamu baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na kufahamu mambo mengi yanayohusu usajili wa timu na alikuwa anajibiwa na mtendaji huyo lakini pia kulikuwa na meseji za watendaji wengine ambao zilionyesha wakiulizana baadhi ya mambo na mtendaji huyo,” kilisema chanzo hicho.

      Delete
    2. Tarehe 7 hutacheza peke yako usije ukaikana kauli yako..

      Delete
  6. Kikulacho hakipo mbali kipo nguoni mwako

    ReplyDelete
  7. Kikulacho hakipo mbali kipo nguoni mwako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic