May 12, 2019


MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Said Khamis 'Jr' amesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wanapambana ili kusalia kwenye Ligi Kuu Bara, msimu ujao.

Jr ametupia mabao tisa mpaka sasa kwenye ligi ambapo wamecheza michezo 35 wana pointi 43 nafasi ya 11.

Akizungumza na Salehe Jembe, Jr amesema kuwa kwa sasa wanatazama namna bora itakayowafanya apate matokeo chanya kwenye michezo yao mitatu iliyobaki.

"Bado hatupo salama kwa sasa kutokana na ushindani ambao upo kwenye ligi kwa sasa, tunatazama namna ambayo itatufanya msimu ujao tubaki ndani ya ligi kwani ni malengo yetu ya kwanza.

"Wachezaji tunapambana kwa hali na mali kutimiza malengo yetu tuna imani kila kitu kitakuwa sawa, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Jr.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic