February 1, 2021


KLABU ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kesho itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya TP Mazembe.

Januari 30, Azam FC ilishinda mabao 3-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10 jioni.

Mabao ya Azam FC mawili yalifungwa na nyota wao Prince Dube na moja lilifungwa na Mudathiri Yahaya huku lile la KMC likifungwa na Lusajo Mwaikenda.

Kesho Februari 2 Azam FC inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya miamba ya Afrika, TP Mazembe ambao ni washindi wa tatu wa mashindano ya Simba Super Cup.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo ya mchezo huo ni kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo inatarajiwa kucheza Februari 7 na Simba ambao ni mabingwa wa Simba Super Cup, Uwanja wa Mkapa.

8 COMMENTS:

  1. Natumaini mashabiki wa mazembe wabongo, mapokezi fc wataenda kuipa tafu timu yao

    ReplyDelete
  2. Unakosa kumbukumbu au ulikuwa hujafika mjini? Timu ya kwanza kuipokea Mazembe, hadi wakanunua jezi ni Mikia FC, walipokuja kucheza na Yanga kwenye group stage ya CL; upo? Waulize uliowakuta mjini.
    Kinachotokea sasa wajuzi hukuita "whatever goes around comes around"

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba ilicheza na TP Mazembe kwenye CAF CCL kabla ya Yanga.Yanga wakawapokea na kununua jezi za TP Mazembe.Yanga alivyocheza na TP ilibidi Manji awaingize mashabiki wote bure uwanjani ili kuwazuia mashabiki wa Simba wasiingie uwanjani.Yanga ikachezea kichapo Kwa Mkapa.Usijasahulishe.

      Delete
    2. Mkumbushe inaelekea kazaliwa juzijuzi au kaanza kushabikia mpira juzi

      Delete
  3. Hamna timu yeyote isipokuwa Utopolo iliyokwenda Airport kupokea wageni.
    Kushangilia is another case lakini kuwapokea ni a step further.
    Ndio maana mnaitwa Mapokezi FC.
    Tabu yenu mnawapokea lakini hamuwasindikizi wakimaliza kucheza.
    Vipi propoganda za kuwalisha uongo wageni bado zinaendelea?

    ReplyDelete
  4. inajulikana wazi...hata wachezaji wao wa kigeni wakiwasili wanaenda kuwapokea kwa wingi uwanja wa ndege ...kama walivyofanya kwa Fiston...Utopolo bwana kazi ni kupokea tu..
    Al Hilal na TP mazembe bado wako bongo ombeni basi mechi ya kirafiki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic