Baada ya
kupoteza mchezo wa jana wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuchapwa mabao 3-1 na
Bayern Munich, hakuna ujanja na nafasi ni ndogo kwa Arsenal kusonga.
Iwapo
itashindwa kusonga, kinachoonekana sasa katika timu hiyo kinatakiwa ni makombe
na si kingine. Kwani kama fedha wanazo.
Kweli kama
watafikia uamuzi wa kubadili kocha msimu ujao, chaguo sahihi la Arsenal
litakuwa ni Jose Mourinho ingawa kuna mambo mengi watalazimika kuyabadili.
Kwanza ni
klabu kutokuwa tayari kutoa mamilioni kununua wachezaji, kitu kizuri ni kwamba
Mourinho si mtumiaji wa mafedha sana, lakini ni tofauti na Wenger.
Tokea
mwaka 2003 alipotwaa ubingwa wa Ureno akiwa na FC Porto, kila mwaka amekuwa
akichukua kikombe katika kila ligi aliyokuwa anafundisha timu fulani.
Mourinho
aliahidi ubingwa tokea siku ya kwanza alipotua Chelsea, kweli alifanya hivyo
ikiwa ni pamoja na kuchukua ubingwa wa Kombe la FA, pia wakafika fainali ya
ligi ya mabingwa na kushindwa kwa penalti na Man United jijini Moscow.
Kama
wanataka kuendelea kubana matumizi, Arsenal hawana ujanja wanaweza kuendelea
kubaki na Wenger, kama ni vikombe, hakuna ujanja, Mourinho ambaye mambo yake
hayaendi vizuri Madrid, ndiye chagu sahihi.
0 COMMENTS:
Post a Comment