Baada ya
kuhaha kwa zaidi ya wiki moja na nusu akitaka kulipwa fedha zake dola 32,000
kutoka kwa uongozi wa Simba, hatimaye ‘zali’ limemuangukia.
Milovan
raia wa Serbia, ameahidiwa kulipwa fedha zake na makamu mwenyekiti wa kamati ya
fedha, Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki.
Mwanamama
huyo jana alikata mzizi wa fitina na kupitisha kumlipa Milovan kwa fedha zake
huku akisema ameamua kuiondolea Simba aibu.
“Simba
ina mambo mengi, lakini sasa hakuna kinachoendelea. Leo wanachama
wanachanganyikiwa, hawajui wapi pa kushika. Mambo hayaendi vizuri kwenye klabu,
huku kocha huyu anadai.
“Sasa
anzunguka tu mitaani anasema maneno, kweli anadai haki yake, kwa nini tusimpe.
Mimi sipendi ubabaishaji, nitamlipa,” alisema Rahma.
Baada ya
mazungumzo ya takribani dakika nne na Rahma aliomba namba za akaunti ya Milovan
na kuahidi kumtumia fedha zake ndani ya siku tatu.
Rahma
ambaye aliondoka jana nchini kwenda Oman, alisema atatuma fedha hizo kwa
Milovana na kumtaka awe na subira hadi atakapotua Oman leo usiku.
Milovan
ambaye alikuwa kama ameshangazwa na hali hiyo kwa kuwa kesho alipanga kutua TFF
kufikisha mashitaka yake, alisema amefurahishwa sana na Malkia wa Nyuki.
Pamoja na
kumlipa, Malkia wa Nyuki aliutaka uongozi wa Simba kufanya mambo kwa uwazi na
usahihi.
“Sidhani
kama ni sahihi watu wanafanya mambo kwa kulipua tu, nafikiri huu ndiyo wakati
mzuri wa wao kuamua kushughulika na timu au kwenda kwenye siasa.
“Mwendo
wa Simba si mzuri, huyu kocha hauwezo kujua inawezekana kesho tukamhitaji tena,
tunachofanya hiki si sahihi.
“Nataka
niwaambie kitu, mimi si mtu wa kubabaishwa, simhofii mtu yoyote na ninafanya
mambo yangu kwa mpangilio. Hiyvo nataka kufanya kazi na watu walio makini,”
alisema.
Milovan
aliyeanza kwa mara ya kwanza kuifundisha Simba mwaka 2008, alikuwa amepanga
kutua TFF kesho kufungua mashitaka yake.
Viongozi
wa Simba, Jumapili iliyopita walikimbia uwanjani mara baada ya timu yao kupata
kipigo cha bao moja kutoka kwa wageni wao Recreativo Libolo ya Angola.
Hali hiyo
imezua mjadala mkubwa, kwamba kwa nini kama viongozi walikimbia wakati jahazi
linazama? Lakini timu inaposhinda wanabaki na kusherekea ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment