February 21, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ametuma salamu kwa wapinzani wao Azam FC kwamba mechi ya Jumamosi watakuwa katika wakati mgumu.
Brandts ambaye kikosi chake kimejichimbia mjini Bagamoyo kujiandaa na mechi gumzo ya Ligi Kuu Bara, amesema ana imani mchezo huo utakuwa mzuri na wa kuvutia, lakini wao wanachotaka ni pointi tatu.
“Sina hofu na kikosi changu, tumekuwa tukiendelea na mazoezi vizuri. Kama binadamu kuna mambo kadhaa yanaweza kutufanya tusifikie tunachotaka, lakini pointi tatu bado ni muhimu sana kwetu.
“Bado tunaiheshimu Azam FC kama moja ya timu bora kabisa, lakini nimewaambia vijana wangu kikosi chetu ni bora zaidi na ushindi ni muhimu hasa Jumamosi.
“Ushindi wa Jumamosi ni hesabu bora kabisa kwetu, kikosi kinaturuhusu kufanya vizuri. Lakini nimesisitiza umakini na kutumia nafasi tutakazozipata ili baadaye tusijalaumu,” alisema Brandts raia wa Uholanzi.
Mchezo huo umekuwa gumzo kubwa miongoni mwa wapenda soka, kila upande ukiamini ukishinda ndiyo safari ya kuufuata ubingwa.
Kila timu ina pointi 36 ingawa Azam FC wana mchezo mmoja zaidi, wakati Yanga ina mchezo mkononi lakini Brandts amesisitiza ushindi lazima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic