February 22, 2013

 

MLEZI wa Simba, Rahma Al Kharusi amefanya kufuru baada ya kumlipa kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic fedha zaidi ya alizokuwa anadai.
Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki amemlipa Milovan dola 35,000 (Sh milioni 56) wakati alikuwa anadai dola 32,000 (Sh milioni 51.2).

Akizungumza jana kutoka Muscat, Oman, Malkia wa Nyuki alisema ameamua kulipa dola 3,000 (Sh milioni 4.8) zaidi ili kocha huyo aweze kulipa deni la hoteli anayokaa.
“Nilihofia wasije wakamsumbua kuhusiana na kulipa hoteli, kama watamlipia basi hiyo dola 3,000 yeye anaweza kutumia katika mambo yake mengine,” alisema.

“Nataka akiondoka aende kwa amani, hakuna haja ya kugombana na watu, kwa mujibu wa taratibu za benki, ikifika Jumatatu yeye aende tu akaangalie akaunti yake.”

FOMU YA MALIPO...

Malkia wa Nyuki aliahidi juzi kumlipa Milovan deni hilo baada ya uongozi wa Simba kuwa umemzungusha huku viongozi wake wakuu wakimkimbia kocha huyo aliyekuwa anadai mshahara wa miezi mitatu kwa ajili ya kuvunja mkataba na mwezi mmoja aliokuwa anadai.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic