February 21, 2013




Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi sasa amehamishiwa katika kitengo cha kuongeza nguvu na ameanza mazoezi ya gym.

Benchi la ufundi la timu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia, limempeleka Okwi na baadhi ya wachezaji katika gym ya timu hiyo.

Pamoja na mazoezi ya gym, Okwi amekuwa akiendelea kufanya mazoezi na wenzake kwa kucheza nao mpira ingawa bado hajaanza kucheza mechi za timu hiyo.

Hivi karibuni, Okwi ambaye alikuwa tegemeo la ushambuliaji katika kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara, Simba alisema ataendelea na programu ya mazoezini pembeni kabla ya kuanza kucheza.

Tokea ametua nchini humo, Okwi hajaanza kuichezea timu hiyo zaidi ya kuendelea na mazoezi. Kawaida amekuwa akicheza mechi za mazoezini ambazo zinahusisha wachezaji wa timu hiyo.

Haina shaka, Mganda huyo akianza kucheza ataonyesha makali aliyonayo ambayo yaliushawishi uongozi wa Etoile du Sahel kutoa kitita cha dola 400,000 kumsajili.
Okwi ambaye analamba mshahara wa dola 15,000 kwa mwezi alilipwa dola 100,000 kwa ajili ya usajili, huku Simba ikipata dola 300,000 ingawa kumekuwa na taarifa Msimbazi walikamata ‘mahela’ zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic