February 21, 2013




Baada ya kuamka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Prisons ya Mbeya jana, mabingwa wa soka Tanzania, Simba wameamua kupasha ‘msuri’ kwa kubaki mjini humo.

Leo jioni, Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi cha Mbeya City ambacho kimepanda daraja hadi Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo amethibitisha Simba kubaki Mbeya na kucheza mechi ya kirafiki.

“Tumeamua kufanya mazoezi kidogo, baada ya hapo tutaondoka kurudi Dar. Tunajua hii ni sehemu ya mazoezi nab ado kuna makosa tunaendelea kurekebisha,” alisema Julio.

Pamoja na kufanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Galatasaray jana usiku, Schalke 04 wametishia kumkatia rufaa mshambuliaji Didier Drogba.

Schalke 04 wametangaza kukata rufaa Uefa kuhusiana na Galatasaray kumtumia Drogba katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, Schalke 04 wameonekana kuficha ‘silaha’ wanayoitumia baada ya kushindwa kuweka wazi tatizo ni lipi.

Drogba anaonekana kutokuwa na tatizo la kuichezea timu hiyo kwani tokea aipe ubingwa Chelsea, hajawahi kucheza michuano hiyo na aliondoka kwenda kujiunga Shanghai Shenhua ya China.

Hata hivyo kuna taarifa, Schalke wanaweza kutumia kipengele cha Shanghai Shenhua kusisitiza bado ina mkataba na Drogba.

Drogba aliichezea Galatasaray mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa dhidi ya Schalke na matokeo yalikuwa sare ya 1-1. Anategemea kuiongoza klabu yake hiyo mpya katika mechi ya marudiano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic