TIMU
tatu za England, Chelsea, Tottenham Hotsupr na Newcastle zilisonga mbele kutoka
hatua ya 32 Bora ya michuano ya Europa, isipokuwa Liverpool tu ndiyo iliteleza.
CHELSEA:
Chelsea
ilipita baada ya sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Sparta Prague, bao lililofungwa katika dakika za
nyongeza na Eden Hazard na kuacha majonzi kwa wageni ambao walianza kuamini
mambo bado wako katika kuwania kusonga mbele. Mechi ya kwanza, Chelsea
ilishinda bao 1-0.
SPURS:
Ikiwa Ufaransa, Spurs ilifanikiwa
kusonga mbele dhidi ya Lyon baada ya sare ya bao 1-1. Kiungo wake Mbeligiji, Mousa
Dembele alifunga bao katika dakika ya 89 na sekunde 30.
Kutokana na sare hiyo, Spurs
imesonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-2 kwa kuwa katika mechi ya
kwanza mjini London ilishinda kwa mabao 2-1.
LIVERPOOL:
Liverpool
iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Zenit
St Petersburg mawili yakiwa yamefungwa na Luis Suarez na Joe Allen, lakini kosa
la beki mkongwe Jamie Carragher lililosababisha wageni wapate bao moja kupitia Hulk, ‘likawakosti’.
Awali ikiwa ugenini,
Liverpool ililala kwa mabao 2-0, hivyo kufanya kuwe na usawa wa mabao 3-3 lakini Zenit St Petersburg wakapita kwa faida ya bao la
ugenini.
NEWCASTLE:
Newcastle
ilisonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Metalist Kharkiv ya
Ukraine, mfungaji akiwa ni Shola Ameobi kwa mkwaju wa penalti. Baada ya mechi
hiyo, vurugu ziliibuka na mashabiki Waingereza wakashambuliwa na wenyeji wao.
Vurugu
pia zilitokea mjini Lyon wakati mashabiki Waingereza wa Spurs waliposhambuliwa.
Hata hivyo ilielezwa Waingereza hao walikuwa chanzo cha vurugu kutokana na
kuonyesha ubabe licha ya kuwa ugenini.
EUROPA RATIBA HATUA YA 16 BORA
Anzhi
Makhachkala v Newcastle
Basle v
Zenit St Petersburg
Benfica v
Bordeaux
Levante v
Rubin Kazan
Steaua
Bucharest v Chelsea
Stuttgart
v Lazio
Tottenham v Inter Milan
Viktoria
Plzen v Fenerbahce
MECHI ZITACHEZWA MACHI 7 NA 14, 2013
0 COMMENTS:
Post a Comment