February 21, 2013




Wababe wa Uturuki wakiwa nyumbani, usiku wa kuamkia leo Alhamisi walishindwa kuonyesha cheche zao baada ya kulazimishwa sare.
Galatasaray walikuwa nyumbani Istambul kuwakaribisha Wajerumani, Schalke 04 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 Bora iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kwa mara ya kwanza, Didier Drogba aliichezea timu yake hiyo mpya katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini hakufanikiwa kufunga.
Wenyeji walipata bao la mapema kupitia kwa Burak Yilmaz lakini Jermaine Jones akasawazisha ‘usiku’ na kuwafanya Galatasaray kuwa na kibarua kigumu katika mechi ya marudiano nchini Ujerumani.
Kama ilivyo kawaida yao, mashabiki walijitokeza kwa wingi Turk Telekom Arena kuishangilia timu yao lakini Wajerumani hao ambao wanaonekana kuwa tishio katika michuano hiyo walionekana kuwa wabishi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic