FIFA WATUA NCHINI, WAFUATA NYASI BANDIA
NYAMAGANA, MWANZA
Ofisa Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Ashford Mamelodi amewasili leo kwa
ajili ya kufuatilia shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Mamelodi,
ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za maendeleo nchini Tanzania
tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, pia amekuja kumtambulisha msaidizi
wake, Patrick Onyango aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.
Wakiwa
nchini, wawili hao wanatarajiwa kupata taarifa ya maendeleo ya mradi wa kuweka
nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, baada ya FIFA kuipa
Tanzania mradi wa nne (GOAL Project 4) wa kuweka miundombinu kusaidia maendeleo
ya mpira wa miguu.
Mwanza
ilipata mradi huo baada ya Halmashauri ya Jiji hilo kukubali masharti ya mradi
huo ya kulipia nakisi ya fedha zinazolipwa na Fifa, ambazo ni sh. milioni 700.
Mradi huo wa kuweka nyasi bandia Nyamagana utagharimu sh. milioni 900, hivyo
nakisi y ash. milioni 200 italipiwa na Jiji la Mwanza.
Pia
Mamelodi na Onyango watapata taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa
Gombani uliowekwa nyasi za bandia kwa msaada wa Fifa katika mradi wa
GOAL Project 3; na pia kupata mikakati ya maendeleo ya TFF kwa mwaka 2013,
ikiwa ni pamoja na kozi na semina mbalimbali zitakazofanyika nchini mwaka huu.
Mamelodi
na Onyango pia watapata taarifa ya maendeleo ya uboreshaji wa mashindano
ya Copa Coca-Cola baada ya Fifa kuingia rasmi kwenye mashindano hayo mwaka jana
kwa kuendesha kozi kwa walimu wa timu za kombaini ya mikoa na waamuzi.
Kwa sasa
mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17, lakini Fifa
inataka yahusishe umri mdogo zaidi ili kuendeleza soka ya vijana na
kushirikisha kikamilifu shule. Maofisa hao wataondoka nchini Jumatatu
asubuhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment