February 24, 2013




Kipa namba moja wa Simba na timu ya taifa, Juma Kaseja ameungana na wachezaji nyota wa duniani kwa viatu vyake kuandikwa jina.
Wachezaji wengi nyota kama Lionel Messi, Ronaldo, Wayne Rooney na wengine kibao viatu vyao vimekuwa na majina yao kama ilivyo katika jezi.
Ingawa si kitu cha kawaida kwa wachezaji wa Tanzania kuonekana viatu vyao vikiwa na majina yao.

Kaseja alionekana akiwa na kiatu aina ya Nike chenye jina lake wakati Simba ilipoivaa Libolo ya Angola na kulala kwa bao 1-0.
Hii si mara ya kwanza mchezaji huyo maarufu zaidi katika kipindi cha miaka mitano nchini kujumuika na wachezaji maarufu.
Hata hivyo haijajulikana mara moja kama Kaseja kapata ‘shavu’ la udhamini wa Nike, au aliamua kufanya utundu mwenyewe na kuandika jina lake.
Hivi karibuni alipata tenda ya kutengeneza tangazo la Pepsi ambalo alijumuishwa katika picha moja na nyota kama Messi, Thierry Henry, Fabregas na wengine kibao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic