February 24, 2013




Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alikuwa rubani wa ndege kwa muda, taarifa ambazo zimezua gumzo.
Imeelezwa Ronaldo mwenye miaka 28, alipata nafasi ya kuiendesha ndege ikiwa angani kwa dakika chache tu. Hata hivyo haijajulikana Ronaldo aliendesha ndege ipi na wapi, hali ambayo imezua maswali mengi.

Taarifa zinaeleza, huenda jambo hilo linafanywa siri kwa marubani waliompa ruhusa hiyo kuonyesha kuhofia adhabu ya kukiuka maadili ya taaluma yao.

Pamoja na marubani hao kuficha, Ronaldo ndiye anaonekana kutibua mambo baada ya kuweka picha katika mtandao wa kijamii wa Twitter akiwa anaendesha ndege hiyo.
Waliotoa maoni, wengi walimtaka kuelekeza mawazo yake katika mechi ya marudiano dhidi ya Man United na si ‘mambo ya kitoto’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic