Swansea City imefanikiwa kuchukua
ubingwa wa Kombe la Capital One kwa kishindo baada ya kuifunga Bradford kwa mabao 5-0 na
kuweka rekodi.
Timu hiyo inayosifika kwa kutandaza
soka la chini ilifanikiwa kutwaa ubingwa, hivyo kuwa timu ya tatu kwa ushindi wa
mabao mengi katika fainali tokea Bury ilipoifunga Derby County 6-0 katika
fainali ya mwaka 1903. Nafasi ya pili ya ushindi mkubwa iko kwa Blackburn
Rovers iliyoshinda 6-1 dhidi ya The Wednesday mwaka 1890.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa
Wembley, London, mabao ya Swansea yalifungwa Dyer na de Guzman (kila mtu
alipachika mawili) na moja akafunga Michu.
Kituko kilitokea ni Dyer na Guzman
kugombea kupiga mkwaju wa penalti, Dyer alitaka kukamilisha hat-trick lakini
mwisho mwenzake ndiye akapewa kazi hiyo ya kuukwamisha mpira wavuni.
de Guzman (kulia) na Dyer wakigombea penalti..
0 COMMENTS:
Post a Comment