Mara baada ya Simba kulala kwa bao
1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, taarifa za kuachia ngazi kwa mwenyekiti wa klabu
hiyo kongwe, Ismail Aden Rage zilienea kama moto wa petrol.
Taarifa hizo zilieleza Rage
alikuwa ameamua kuachia ngazi baada ya kuona mambo yanazidi kwenda mlama.
Hata hivyo, alipozungumza na
Salehjembe, Rage aliruka na kusema hakuna mtu ambaye amezungumza naye kuhusiana
na hilo.
“Kama kuna mtu kakuambia nimefanya
hivyo basi muamini yeye, sina taarifa hizo,” alisema Rage na alipoambiwa
amefanya mahojiano na waandishi, akajibu:
“Sijazungumza na mwandishi yoyote
kuhusiana na kujiuzuru, hapa unavyoona nimeitisha kikao cha kamati ya utendaji
Jumatatu (leo), sasa nitaachia vipi ngazi halafu niitishe kikao.
“Ndiyo maana nakuambia
sijazungumza na mtu yoyote, kwa kifupi naona mambo hayaendi vizuri na kuna watu
wanatusakama, kuna njama tunafanyiwa, hii si hali ya kawaida,” alilalama Rage.
Askari Polisi walilazimika jana
kuwaondoa kwa nguvu uwanjani mashabiki wa Simba ili kuepusha vurugu wakati wao
walidai walitaka kukutana uso kwa uso na Rage na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
Mashabiki hao walikuwa wakilalama
kwamba uongozi mbovu ndiyo unaowafanya wayumbe na kufungwa katika mechi ya jana
dhidi ya Mtibwa Sugar.
Bora akae pembeni tu maana hali ishakuwa si hali kwenye timu na mwenendo ni mbovu hasa sasa asisubiri mpaka wamvunjie heshima kwake....
ReplyDeleteHata tabora tu hawamtaki hahahahahahaha
ReplyDelete