Na Saleh Ally
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brants amesema pamoja na wachezaji
wake kushindwa kufunga bao zaidi ya moja katika mechi tatu mfulizo, lakini timu
nyingi zinacheza mchezo wa kujilinda zaidi.
Brandts amesema Yanga imekuwa ikitahidi kutaka kushinda,
inacheza soka la kuvutia pamoja na kutafuta ushindi wakati wapinzani wao
wanakaa nyuma tu.
“Ukiangalia mechi na Azam FC, asilimia kubwa wachezaji wao
walikuwa wamekaa nyuma na kushambulia kwao ni kwa kushitukiza. Baadaye
tulichezana Kagera Sugar, basi mambo yalikwenda hivyo hivyo.
“Nilifikiri katika mechi na Toto kungekuwa na mabadiliko kidogo,
lakini mambo yalishindikana kabisa, utaona timu imejaza wachezaji wote nyuma,
nafikiri si kitu sahihi,” alisema Brandts.
“Nafikiri soka la Tanzania linapaswa kuwa la ushindani ili
kupiga hatua, lakini aina ya uchezaji ule, hauwezi kuwa sahihi. Tutaharibu
mpira wa Tanzania na mambo hayatakuwa mazuri, waambieni.
“Ushindani ni pamoja na kucheza soka la ushindani, ndiyo
maana umeona kuna makocha wamekuwa wakilaumiwa na kuitwa wanaharibu soka,
wanacheza mpira wa kukaa nyuma tu bila ya kushambulia na kupanga uchezaji ambao
pia unaweza nkuwavutia mashabiki. Hali hii inaniumiza sana.”
Mara nyingi, Brandts
aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi, amekuwa akisisitiza anataka timu
yenye uwezo wa kucheza soka la kujvutia, kushambulia mfululizo na kufunga mabao
mengi.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment