March 4, 2013


Baada ya kufanikiwa kuing’oa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa, Recreativo de Libolo ya Angola sasa itakutana na El Merreikh ya Sudan.

 El Merreikh ni mmoja wa vigogo wa Afrika na hivi karibuni ilikuwa katika harakati za kumnasa Mrisho Ngassa anayekipiga Simba sasa, lakini wakaishia kunawa.


Ingawa Wasudani hao walikuwa tayari kutoa fedha ili kumchukua kiungo huyo na baada ya malumbano Simba na Azam FC wanaomliki kufikia mwafaka na kukubali kumuuza, Ngassa alipotelea kusikojulikana.

Baada ya kuona wanasumbuka bila ya majibu ya kueleweka, Wasudani hao waliokuwa tayari jijini Dar es Salaam, waliamua kurejea kwao na kuchukua uamuzi wa kumchukua mshambuliaji wa zamani wa Simba na APR ya Rwanda, Selemani Ndikumana raia wa Burundi.

Ndikumana alichukua nafasi ya Ngassa na ndiye mmoja wa washambuliaji tegemeo wa timu hiyo ambao sasa ina kibarua cha kuwavaa Libolo ambao wameing’oa Simba kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya kuwafunga 1-0 jijini Dar na 4-0 kwao Calulo, Angola!

zifuatazo ni mechi zote zinazofuata za Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwemo kati ya Libolo na El Merreikh...

Team 1   Agg.   Team 2   1st leg     2nd leg  
Zamalek Egypt A Democratic Republic of the Congo AS Vita Club 15–17 Mar 5–7 Apr
Saint George Ethiopia B Mali Djoliba 15–17 Mar 5–7 Apr
CA Bizertin Tunisia C Zimbabwe Dynamos 15–17 Mar 5–7 Apr
Tusker Kenya D Egypt Al-Ahly 15–17 Mar 5–7 Apr
Zanaco Zambia E South Africa Orlando Pirates 15–17 Mar 5–7 Apr
Mochudi Centre Chiefs Botswana F Democratic Republic of the Congo TP Mazembe 15–17 Mar 5–7 Apr
Vital'O Burundi G Nigeria Enugu Rangers 15–17 Mar 5–7 Apr
Recreativo do Libolo Angola H Sudan Al-Merreikh 15–17 Mar 5–7 Apr
JSM Béjaïa Algeria I Ghana Asante Kotoko 15–17 Mar 5–7 Apr
Primeiro de Agosto Angola J Tunisia Espérance ST 15–17 Mar 5–7 Apr
FUS Rabat Morocco K Cameroon Union Douala 15–17 Mar 5–7 Apr
Séwé Sports Ivory Coast L Sudan Al-Hilal 15–17 Mar 5–7 Apr
AFAD Djékanou Ivory Coast M Cameroon Coton Sport 15–17 Mar 5–7 Apr
Casa Sport Senegal N Mali Stade Malien 15–17 Mar 5–7 Apr
Kano Pillars Nigeria O Republic of the Congo AC Léopards 15–17 Mar 5–7 Apr
ASFA Yennenga Burkina Faso P Algeria ES Sétif 15–17 Mar 5–7 Apr

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic