Wakongwe Liverpool wameendelea
kuchanua baada ya kuichapa Aston Villa kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu
England iliyomalizika hivi punde.
Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa
Park ilikuwa kali na ya kusisimua lakini mwisho wageni Liverpool waliibuka na
ushindi.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Jordan
Henderson katika
dakika ya 47 na nahodha, Steven Gerrard akapiga msumari wa pili kwa mkwaju wa
penalti katika dakika ya 60.
Aston
Villa walipata bao lao la kufutia machozi katika dakika ya 31 kupitia kwa
kiungo wao Cristian Benteke.
0 COMMENTS:
Post a Comment