Muda mchache baada ya kumtimua kocha
wake, Martin O’neill, Sunderland imeanza mazungumza na Paolo di Canio.
Di Canio, kocha wa zamani wa Swindon
Town, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya O’Neill.
Taarifa zinaeleza di Canio amefanya
mazungumzo na mmiliki wa Sunderland, Ellis Short ambaye alikuja hapa nchini na
kuanzisha uhusiano na Simba.
Mazungumzo ya Short na di Canio raia
wa Italia mwenye miaka 44, yamefanyika jijini London mchana huu na dalili
zinaonyesha huenda akachukua nafasi hiyo ya kuikoa Sunderland ambayo inasuasua
kwenye msimamo wa ligi.
Kama watakuwa wamekubaliana, bosi
huyo wa zamani wa Swindon ataanza kazi wakati Sunderland ikiivaa Chelsea katika
Ligi Kuu England Jumamosi ijayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment