March 11, 2013





Michuano ya Kombe na Amani na Upendo imemalizika jana kwa kikosi cha Katoro kutangazwa mabingwa wapya wa michuano hiyo iliyodhaminiwa na gazeti maarufu la michezo la Championi.

Mechi hiyo iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Katoro mjini hapa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, Katoro waliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalty dhidi ya majirani zao Buseresere.

Baada ya muda wa kawaida kwisha, mikwaju ya penalty ikaanza kupigwa na mwisho, Katoro wakaibuka na ushindi wa 5-4 na kukabidhiwa kombe na zawadi ya Sh 500,000.

 Michuano hiyo pia ilihudhuriwa na wachungaji na masheikh wa eneo hilo waliokuwa wametoka katika kikao cha upatanishi kilichoongozwa na Eric Shigongo na Saleh Ally.
Baada ya kikao hicho, viongozi hao walikubali kufuta tofauti zao, wakawataka waumini kudumisha amani.

Michuano hiyo ilianzishwa na gazeti la Championi kwa lengo la kurejesha amani na upendo kupitia michezo ikiwa ni baada ya vurugu za kidini kuibuka, mwislamu mmoja akapigwa risasi na mchungaji akauwawa.

Tofauti zilianzia katika suala la kuchinja, Wakristo wakitaka kuchinja na kuuza buchani na Wakristo wakipinga hilo. Viongozi wa serikali, kuanzia Wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri mfano Wassira na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walishindwa, lakini Mungu akasaidia naShigongo na Saleh wakafanikiwa katika hilo.

Hali haikuwa nzuri sana, lakini mkutano wa upatanishi umeonyesha kurudisha amani na waumini wote wameahidi kushirikiana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic