Beki nyota wa Man United, Rio Ferdinand amelaumiwa kutokana
na kitendo kisicho cha kimichezo alichomfanyia Fernando Torres wa Chelsea.
Ferdinand alimtadika ngumi ya kisogoni mshambuliaji huyo wa
Chelsea wakati mwamuzi akiangalia upande mwingine.
Hali hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka
kwamba kwa umri wake wa miaka 34 hakustahili kufanya kitendo alichofanya.
Vibaya zaidi, Rio hata baada ya kumpiga Torres na kuanguka, bado
alimuinua kikatili huku akimlaumu kama alijiangusha.
Katika mechi hiyo ya jana ya nusu fainali ya Kombe la FA
ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment