March 10, 2013




Cristian Ronaldo ndiye mchezaji anaongoza kwa jezi zake kuuzwa zaidi kwa wachezaji wa mabingwa wa Hispania, Real Madrid.

 Tokea ametua klabuni hapo akitokea Man United ya England, Ronaldo ndiye ameshikilia kasi ya mauzo kwa klabu yake ingawa kama ni La Liga, anapata upinzani mkubwa kutoka kwa wachezaji wa Barcelona kama Messi, Xavi na Iniesta.

Kwa upande wa Madrid, ukiachana na Ronaldo, wengine wanaofuatia ni kipa Iker Casillas ambaye amekuwa akiongoza kundi la wachezaji kutoka Hispania.

Baada ya wawili hao, wengine waliouza zaidi jezi zao kwa misimu miwili sasa ni Wahispania pia ambao ni Sergio Ramos aliyeshika nafasi ya tatu, kiungo Xabi Alonso na Mesut Özil.

Ozil raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki anaonekana kupanda kwa kasi zaidi hadi kufikia kushika nafasi ya tano na amekuwa mmoja wa wachezaji wanaopata mashabiki kwa kasi katika klabu hiyo

Kaka na Benzema ambao walinunuliwa kwa bei kubwa, wanaonekana kushindwa kuwashawishi mashabiki wa Madrid kwa kiwango kizuri ili waweze kununua jezi zenye majina yao.

kAKA 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic