Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji hatimaye ameamua kusema ukweli anavyojisikia kuhusiana na
Ligi Kuu Bara inavyokwenda ukingoni.
Manji
amesema amekuwa na presha kubwa kupindukia kadri Ligi Kuu Bara inavyokwenda
ukingoni hali inayomyima raha.
Akizungumza
na Salehjembe, Manji amesema wakati mwingine analazimika kusimamisha shughuli
zake nyingine Yanga inapokuwa uwanjani.
“Kweli
kuongoza ni kazi kubwa, kila mechi unataka kushinda. Nilisema dhidi ya Azam FC
ilikuwa ni muhimu zaidi, lakini baada ya hapo nikaona dhidi ya Kagera ni ngumu
zaidi.
“Nayo
ikapita, kama tumeshamaliza lakini inaonekana pointi tatu za Toto ndiyo muhimu
zaidi. Utaona kila mechi ni muhimu zaidi na presha inakuwa kubwa sana kila
baada ya mechi moja.
“Wakati
mwingine sitaki hata kuona mechi za Yanga kwa sababu ya presha kubwa, natamani
kuona timu inashinda lakini ligi ni ngumu sana.
“Angalia
pamoja na ubora wa kikosi cha Yanga, hakuna anayeweza kukataa kwamba tuna
kikosi bora kabisa, lakini ushindi wetu sasa ni bao moja tu kwa mechi.
“Jiulize
kwa nini tusishinde nne au tano, maana yake ushindani katika ligi ni mkubwa
sana,” alisema Manji ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu.
Manji kwa kushirikiana na viongozi wenzake, wachezaji pamoja na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ameahidi kupambana ili kuhakikisha Yanga inakuwa bingwa mwishoni mwa msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment