Kocha
Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amewaambia washambuliaji wake bado haridhiki na
kiwango cha ufungaji mabao.
Yanga ina
washambuliaji nyota kama Jerry Tegete, Didier Kavumbagu, Saidi Bahanuzi na
Hamis Kiiza ambao wanaonekana kuishiwa mafuta ya kupachika mabao kwa kipindi
sasa.
Brandts,
beki wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi iliyocheza hadi Kombe la Dunia,
amesema hali ya wachezaji wake kutotumia nafasi za kufunga wanazozipata
inamchanganya.
“Hili si
tatizo la siku moja iliyopita, tumelizungumza sana na mara nyingine kulifanyia
mazoezi.
“Lakini
inaonekana bado, nafikiri sitalaumu kama nilivyosema lakini tutaendelea
kulifanyia kazi kwa kwua nataka Yanga inayofunga mabao zaidi ya matatu kila
mechi ikiwezekana.
“Bado
nina washambuliaji wazuri kabisa ambao wanaweza kufanya hivyo, ndiyo maana
inanichanganya kwa kiasi fulani,” alisema Brandts.
Yanga
imekuwa ikishinda bao 1-0 kila mechi inayocheza katika kipindi ambacho
inahitaji kujikita zaidi kileleni.
Hata
hivyo, mwendo wake wa kuchota pointi tatu kila mchezo, unaonekana kuisaidia
zaidi ingawa kweli inahitajika kufunga mabao zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment