Baadhi ya
wachezaji Simba huenda wakapata maisha nchini Oman kutokana na kuendelea
kufuatiliwa na wakala nchini humo.
Said Al
Maskery ambaye ni mmoja wa mawakala maarufu nchini Oman, amesema amekuwa
akiendelea kuwafuatilia baadhi ya wachezaji wa Simba.
Hivi karibuni,
Simba iliweka kambi ya wiki mbili nchini humo kujiandaa na Ligi Kuu Bara na
michuano ya kimataifa.
Akizungumza moja kwa moja kutoka jijini Muscat, Oman, Al
Maskery alisema kuna baadhi ya wachezaji hasa ambao ni chipukizi, anaendelea
kuwafuatilia na usajili utakapofunguliwa ataangalia cha kufanya.
“Kweli
kuna wachezaji tunawafuatilia taratibu kwa kuwa sasa tuna muda wa kutosha kabla
ya kuanza usajili na tumeanza kufanya hivyo kitambo. Kwa sasa sitawataja majina,” alisema.
“Kama
tutaridhika, basi tutafanya mazungumzo na Simba, pia mchezaji kwa ruhusa ya
klabu. Baada ya hapo klabu inayowataka nayo itafuata taratibu kwa muongozo,”
alisema.
Al
Maskery ambaye amewahi kuwapeleka wachezaji kadhaa wa Simba nchini Oman tokea
miaka ya 1990, alisisitiza, zaidi amekuwa akiangalia wachezaji makinda ingawa
wakati mwingine suala la mahitaji ya timu linampelekea kutafuta mchezaji fulani.
Wakala huyo
amekuwa maarufu sana kwa kuwatafutia wachezaji timu lakini pia makocha
mbalimbali ambao wako chini ya kampuni yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment