LIGI YA VODACOM KUENDELEA JUMAMOSI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa
Tanzania Bara inaendelea Jumamosi (Machi 16, 2013) kwa mechi tatu
zitakazochezwa katika miji ya Mwanza, Dar es Salaam na Manungu, Turiani mkoani
Morogoro.
Toto Africans inayopigana kukwepa kurudi daraja la
kwanza itakuwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kutoka Tanga katika mechi
itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Vinara wa ligi hiyo Yanga wataumana na Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar wakati Uwanja wa Manungu, Turiani utakuwa
mwenyeji wa mechi ya Mtibwa Sugar na Coastal Union.
UCHAGUZI
TAFCA KUFANYIKA MOROGORO
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira
wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma
ambapo wajumbe wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya uchaguzi.
Wagombea waliopitishwa kuwania uongozi na Kamati ya
Uchaguzi ya Tafca chini ya uenyekiti wa
Ramadhan Mambosasa ni Oscar Don Koroso (mwenyekiti), Lister Manyara (makamu mwenyekiti)
na katibu (Michael Bundala).
Wengine ni Gabriel Gunda (katibu msaidizi), Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF (Wilfred Kidao)
wakati wagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Jemedali Saidi, George Komba na
Magoma Rugora.
0 COMMENTS:
Post a Comment