March 12, 2013



Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Kim Poulsen anatarajia kesho  Machi 13, huku kukiwa na matarajio kidogo sana katika mabadiliko.

Mkutano huo wa Waandishi wa Habari utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 24 mwaka huu.

Kama atafanya mabadiliko, basi Poulsen raia wa Denmark itakuwa si zaidi ya asilimia 10, hii inatokana naye kukiamini zaidi kikosi chake kilichocheza mechi tatu za mwisho dhidi ya Cameroon, Ethiopia na Zambia.

Kikosi hicho kilicheza mechi tatu na kushinda mbili zote za nyumbani dhidi ya Zambia na Cameroon, kila timu ililala kwa bao 1-0. Lakini Stars ikapoteza mchezo wake wa kirafiki wa ugenini dhidi ya Ethiopia kwa kufungwa mabao 2-1.

Wachezaji waliocheza katika mechi hizo wana asilimia 98 ya kurejea, halafu itakuwa vigumu kwa Mdenishi huyo kucheza mechi tatu za kirafiki halafu ateue wachezaji wengine.

Mafanikio ya mechi hizo tatu, kunamfanya Mdenishi huyo alazimike kurudisha kikosi kilekile kitakachoongozwa na nahodha Juma Kaseja, licha ya kukaa mechi mbili benchi katika klabu yake ya Simba.

Swali gumu ni kwa wachezaji wawili wa Azam FC, Erasto Nyoni na Aggrey Morris ambao wamesimamishwa na klabu ya Azam FC, hivyo wamekuwa hawachezi huku ikionekana wazi suala hilo linamkera Poulsen na tayari alishawambia anahitaji kuwaona wakicheza.

MECHI TATU ZA MWISHO ZA STARS ZILIZOPITA:
Desemba 22, 2012
Tanzania 1-0 Zambia (Kirafiki)
Januari 11, 2013
Tanzania 1-2 Ethiopia (Kirafiki)
Februari 6, 2013
Tanzania 1-0 Cameroon (Kirafiki)

MECHI TATU ZITUATAZO ZA STARS:
Machi 22, 2013
Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7, 2013
Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14, 2013
Tanzania Vs Ivory Coast (Kufuzu Kombe la Dunia)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic