Kocha
Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema analala kwa shida kubwa, anashindwa kupata
usingizi mzuri kutokana na kutaka kupanga namna ya kuona wafungaji wake
wanabadilika.
Brandts
raia wa Uholanzi amesema washambuliaji wake wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi
sana za wazi, kitu ambacho ni hatari kwake.
Amesema
mara kadhaa amekuwa akifanya mazoezi na kikosi chake kuhakikisha kinatengeneza
nafasi nyingi za kufunga lakini mambo yanaonekana kuwa tofauti kabisa.
“Mara
nyingi nimesikia watu wakisema au magazeti kwamba mimi nawalaumu wafungaji
wangu, siwezi kufanya hivyo kwa kuwa kulaumu si njia nzuri ya kutatua tatizo. Nafikiri
hujawahi kuniona hata nikilaumu wachezaji uwanjani.
“Nakosa
usingizi mzuri, maana nataka kuona wanafunga kwa sababu wana uwezo wa kufanya
hivyo. Tunatengeneza nafasi nyingi sana za kufunga lakini hatuzitumii.
“Ukiangalia
nina washambuliaji bora kabisa, Tetege, Saidi (Bahanuzi), Didier (Kavumbagu) na
Hamis (Kiiza), tunastahili kuwa na mabao mengi zaidi.
“Utaona
mazoezi ya leo tunachofanya ni namna ya kufunga, krosi za juu na chini. Namna ya
kutulia, ingawa bado tunapata shida kutokana na uwanja wenyewe,” alisema
Brandts.
Kavumbagu
ana mabao tisa, wakati Jerry aliyeibuka katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
Bara, ana mabao saba. Washambuliaji hao wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi za
kufunga.
Katika
mechi mbili zilizopita za Yanga, walipoteza zaidi ya nafasi kumi na kiungo
Niyonzima ndiye aliwaokoa kwa kufunga katika mechi hizo dhidi ya Azam FC na
Kagera Sugar ambazo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 kila mechi.
0 COMMENTS:
Post a Comment