Makamu
Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ametangaza kuachia nafasi yake
hiyo.
Kaburu
ameamua kuachia ngazi ikiwa ni saa chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili, Zacharia Hans Pope kubwaga manyanga.
Habari za
Kaburu kujiuzulu zimethibitishwa na uongozi wa Simba, ingawa mwenyewe
hakupatikana kulizungumzia hilo.
Katibu
Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amethibitisha hilo jana alipozungumza na Blog
namba moja ya michezo nchini Tanzania ya Salehjembe.
“Ni kweli
Kaburu amejiuzulu na tayari tumeshaueleza umma kuhusiana na hilo, amechukua
uamuzi huo na kutoa taarifa kwetu,” alisema Mtawala.
Kuondoka
kwa Hans Pope na Kaburu ambao wote ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba,
kunamuweka Mwenyekiti, Ismail Aden Rage katika wakati mgumu.
Kutokana
na mwenendo wa Simba, Rage amekuwa akishinikizwa kujiuzulu, ingawa amekuwa
mgumu kama ‘nyundo’.
0 COMMENTS:
Post a Comment