Domayo (kushoto) akiwania mpira na Nurdin ambaye pia anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa goti ndani ya wiki hii...
Kiungo kinda wa Yanga, Frank Domayo sasa ana jina jipya ambalo limetokana na uwezo mkubwa wa kupiga pasi anapokuwa anakichezea kikosi hicho.
Domayo
amekuwa akipiga pasi za uhakika anapocheza katika mazoezi ya timu hiyo, lakini
amekuwa bora zaidi katika mechi za Yanga.
Kutokana
na kuonyesha uwezo huo, wenzake wamembandika jina la chumvi, wakiwa na maana
ndiye anayenogesha mambo kama kiungo chumvi katika mboga.
Awali
ilikuwa kazi kuelewa maana ya chumvi kutokana na maneno mengi ya Kiswahili
kubadilishwa maana na vijana wa mjini.
Lakini baadaye
wachezaji hao walifafanua kuwa chumvi imetokana na uwezo huo wa kupiga pasi
safi zenye ‘macho’.
Kocha
Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts naye alijikuta akiungana na wachezaji wake na
kumuita jina hilo.
Wakati Domayo
ambaye ni mtaratibu akiondoka mazoezini, Brandts alimuita: “Chumvi, how are
you.” Hali iliyosababisha watu waliokuwa eneo hilo waanze kucheka.
Pamoja na
kuwa kinda, Domayo tayari ni tegemeo kwa Yanga na Taifa Stars, yote inatokana
na uwezo mkubwa na utulivu wake uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment