Mshambuliaji Kun Aguero wa Man City huenda akakumbana na adhabu kali kutoka FA iwapo atabainika alimkanyanga kwa makusudi beki wa Luiz wa Chelsea.
Aguero ambaye ni raia wa Argentina alimrukia Luiz kwa miguu miwili wakati timu zao zilipokutana katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA.
Katika mechi hiyo, Chelsea ikiwa nyumbani Stamford Bridge, ililala kwa mabao 2-1 na Man City ikasonga hadi fainali.
Picha zinaonyesha Aguero akiwa amemrukia Luiz kwenye makalio baada ya beki huyo raia wa Brazil kuanguka wakati akiwania mpira na Muargentina huyo.
Tayari imeelezwa, FA imeanza kulifanyia kazi suala hilo la Aguero na Luiz na kama itabainika ilikuwa ni makusudi, basi huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa mechi kadhaa.









0 COMMENTS:
Post a Comment