Kocha Mkuu wa Man United, Alex Ferguson amesema mshambuliaji wake Robin van Persie nusura amtoe uhai.
Ferguson alisema van Persie alimkumbatia kwa nguvu kupita kiasi hali iliyomfanya ashindwe kupumua kwa muda.
Van Persie alimkumbatia kwa nguvu baada ya timu kufunga bao la penalti katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi Stoke City, jana.
Kabla ya hapo, van Persie ambaye amekuwa moto mkali kwa kupachika mabao alikuwa hajafunga bao katika mechi 10 mfululizo.
Hali hiyo ilionyesha kumchanganya, hivyo katika mechi hiyo ya jana ambayo United walishinda kwa mabao 2-0, van Persie alionyesha furaha ya ajabu.
Lakini Ferguson akasema: “RVP nusura aniue, alinikumbatia kwa nguvu sana hadi nikashindwa kupumua. Alijisahau kuwa nina miaka 71.”









0 COMMENTS:
Post a Comment