Klabu ya Manchester United iko katika hatua za
mwisho za kumnasa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski kwa
kitita cha pauni milioni 25.
Tatizo kubwa wapinzani wa Dortmund, Bayern Munich
nao wametoa dau sawa na la Man United hivyo kufanya mchezo uwe mgumu.
Kocha Mkuu wa Man United, Alex Ferguson ambaye
amekuwa akimuwania mchezaji huyo kwa miezi 18 sasa, anataka kumtumia raia huyo
wa Poland kama pacha wa Mholanzi, Robin van Persie iwapo kila kitu kitakwenda
safi.
Mabao yake manne dhidi ya Real Madrid katika mechi
ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa imezidisha nguvu ya timu hizo mbili
kuhakikisha zinamnasa kwa ajili ya msimu ujao.
Mashabiki wa Dortmund wanaona ni bora mshambuliaji
huyo kama atatua man United kuliko kwenda kwa wapinzani wao hao ambao tayari
watamchukua mshambuliaji wao mwingine machachari, Mario Gotze kwa kitita cha
pauni milioni 23.
Hata hivyo, United wamekuwa na hofu huenda Lewandowski
akaamua kubaki Ujerumani na kutua Bayern kwa kuwa kuna taarifa za kusaini
mkataba wa awali na klabu hiyo ya Magharibi mwa Ujerumani.
Suala la mashabiki wa Dortmund kutokuwa na furaha kama Lewandowski
atabaki na kucheza Bayern ndiyo imekuwa silaha ya Ferguson akisisitiza bora
angecheza nje ya Ujerumani kuepuka kuwaumiza.








0 COMMENTS:
Post a Comment