Ingawa Ligi Kuu England inaenda ukingoni, Liverpool imeamka na kuichaoa
Newcastle ikiwa nyumbani kwa mabao 6-0.
Huku ikicheza bila ya mshambuliaji wake nyota, Luis Suarez ambaye
amefungiwa kutokana na kumuuma Branislav Ivanovic wa Chelsea, Liverpool ilipata
mabao mawili kupitia kwa Agger na Henderson.
Kipindi cha pili ndicho kilikuwa cha mauaji baada ya Danny Sturridge
alifunga mabao mawili, Henderson akaongeza moja na Borini aliyeingia kipindi
cha pili akafunga moja.
Newcastle ilipata pigo baada ya beki wake Debuchy kulambwa kadi nyekundi
baada ya kupata njano ya pili.
Mabao hayo yaliyoonekana kama aibu kwa mashabiki wa Newcastle
yaliwafanya waanze kuondoka.
Kuanzia bao la nne, mashabiki wa Newcastle walianza kuondoka kwenye
Uwanja wa St James Park kuonyesha hawakubaliani na hali hiyo.
Kila bao lilipofungwa kuanzia hapo, idadi ya mashabiki ilijikusanya na
kutoka uwanjani hapo kuonyesha kuchukizwa kupita kiasi.
Baada ya bao la tano, Liverpool ilianza mchezo wa ‘kujiburudisha’ huku
ikipiga basi fupi fupi.
MATOKEO MENGINE LIGI KUU ENGLAND LEO
Man City 2...1 West Ham
Everton 1... 0 Fulham
Southampton 0... 3 West Brom
Stoke 1...0 Norwich
Wigan 2...2 Spurs











0 COMMENTS:
Post a Comment