April 17, 2013



Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar.
Bi Kidude alikuwa akiuguzwa huko Bububu kwa muda mrefu na sasa ni gumzo kuhusiana na umri wake.
Lakini taarifa za watu wengi wanamkadiria kuwa alifikisha miaka 102 hadi mauti yalipomkuta leo.
Wakati fulani, wakati wa uhai wake, Bi Kidude alimuambia Salehjembe kwamba anachotakiwa kujua ni kwamba alizaliwa kabla ya Julius Nyerere.
Huo ndiyo ulikuwa utambulishi wake wa alizaliwa lini akionyesha kutotambua hasa siku, mwezi na mwaka aliozaliwa.
Taarifa kutoka kwa ndugu zake zimeeleza mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho.
Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi maarufu katika eneo hilo.
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao na alionyesha kipaji cha hali ya juu.
Mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi umri kwa kiasi kikubwa sana.

Bi Kidude pia liwahi kuimba na mwimbaji maarufu wa taarabu, Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote duniani.
Hesabu inaonyesha, Bi Kidude ndiye msanii mkongwe wa Tanzania aliyezunguka sehemu mbalimbali duniani akiimba na ameimba katika majukwaa mengi zaidi na wasanii maarufu duniani kote kuliko msanii yoyote wa Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic