April 14, 2013





Chelsea ya London, England imekuwa ndiyo timu maarufu inayoongoza kuajiri na kufukuza makocha maarufu kabisa duniani.

Ndani ya kipindi cha miaka 10, Chelsea imeajiri na kufukuza mameneja 10 maarufu ikiwa na lengo la kutaka kupata Kombe la Ligi ya Mabingwa.
Juhudi za Mrusi, Roman Abramovich anayeimiliki Chelsea kutaka kulipata kombe hilo zimekuwa zikigonga mwamba.



Si wote walitimuliwa, lakini wote waliaahiriwa na baadaye kuachana au kufukuzwa na Chelsea. Makocha hao ni Claudio Ranieri, Jose Mourinho, Avram Grant, Ousted: Luiz Felipe Scolari, Ray Wilkins, Guus Hiddink, Departed: Carlo Ancelotti, Andre Villas-Boas, Roberto Di Matteo na sasa iko na Rafael Benitez.
 
Kuna taarifa amekuwa akifanya juhudi na huenda akamrudisha kocha Jose Mourinho ambaye aliondoka Chelsea akiwa amefanikiwa kuifikisha fainali lakini ikafungwa kwa mikwaju ya penalti na Man United.

Chelsea imekuwa ni moja ya timu zilizobadilika na kuwa tishio wakati wa utawala wa Mrusi huyo mwenye utajiri wa mafuta.

Lakini wataalamu wa mambo wanaamini hata kuajiri na kuwatimua makocha maarufu imekuwa ni sehemu ya kuifanya klabu hiyo ya London izidi kwua maarufu katika kipindi kifupi tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic