FULL TIME:
Dk 90 plus 1 Sunzu anapambana na Mieno lakini
anashindwa kuuwahi mpira. Kiasi fulani timu zote zinaonekana zimeridhika na
sare.
Dk 90, mwamuzi wa akiba anaonyesha dk 4 za nyongeza.
Dk 81, Simba wanamtoa Ngassa anaingia Sunzu, Azam
wanamtoa Mieno anaingia Jabir Aziz
Dk 80, Azam wanamtoa Bocco anaingia mkongwe Abdi Kassim
Babi
Dk 79, krosi safari ya Waziri nusura imkute Bocco
lakini Mudde anafanya kazi ya ziada.
Dk 75 Simba wanamtoa Chanongo anaingia Edward Christopher
GOOOOOO...Dk 70 Mcha anapiga mpira wa adhabu ambao unamgonga beki na kukumkuta beki wa
Simba, unamfikia Mieno na kuandika bao la kusawazisha.
Dk 68, Tchetche anaangushwa kwenye eneo la nje ya
18, Mudde analambwa kadi nyekundu.
Dk dk 66, Simba wanapa kona baada ya shuti la Lucian
kumgonga mchezaji Azam, haijazaa matunda.
Dk 62, Simba wanapata kona baada ya shuti la Ngassa
kumgonga Atudo, Azam wanaokoa
DK 56 Azam wanaendelea kulishambulia lango la Simba,
pasi nzuri ya Mcha, Bocco anashindwa kumalizia.
Dk 50 Dhaira anaonekana kupoteza muda...
Dk 49, Azam FC wanafanya shambulizi, lakini Tchetche
anashindwa kuufikia.
HALF TIME:
Dk 41-44, timu zinatumia muda mwingi zikicheza
katikati ya uwanja, mashambulizi yanakuwa ni dhaifu.
Dk 39, dhaira anafanya kazi ya ziafa, inakuwa kona
ambayo inapigwa na kuwa kona tena, inapigwa, Simba wanaokoa.
Dk 36 Mwamuzi Mbaga anatoa kadi ya njano kwa Seseme
wakati aliyecheza faulo ni Chollo.
DK 33, Mwamuzi Oden Mbaga anamtoa nje Kocha Hall wa
Azam FC kutokana na kumfokea mshika kibendera naye yeye pia.
GOOOOOOO DK 29 Tchetche anapiga bao
Dk 29, Lugiani anamuangusha Mcha ndani ya eneo la
hatari...PENAAAAAAT
Dk 20, Azam wanafanya mabadiliko, anatoka Kakolaki
anaingia Mcha
GOOOOOO dk 18, Ngassa anawachambua mabeki wawili wa
Azam Fc na kutoa pasi kwa Singano Messi ambaye anafunga kwa ulaini kama penalti
Dk 17, Kocha Stewart Hall anamsimamisha Mcha hamis
aanza kupasha misuri
Dk 16, Azam wanazidi kushambulia kwa kuwa Simba
wamerudi nyuma, krosi ya Tchetche inatua kwa Bocco lakini anakua mzito
DK 14, Sure boy anapiga shuti kuuuubwa akiwa karibu
na lango.
GOOOOOOOO..DK 11, Singano ‘Messi; anafunga bao safi
baada ya pasi nzuri ya Ngassa.
Dk 9, Azam wanajibu, lakini Tchetche anakuwa mzito,
Kapombe anaokoa.
Dk 8, Simba wanafanya shambulizi kali, krosi ya
chini ya Ngassa anaikosa Kiemba, hatua tatu kutoka langoni.
Dk 6, mpira wa krosi wa Ngassa unatua kwa Chanongo
lakini anashindwa kuupiga vizuri.
Dk 2 Simba wnafanya shambulizi lakini Chanongo
anashindwa kumalizia mpira.
SIMBA
Dhaira, Chollo, Mdigo, Mudde, Seseme, Lugiani,
Chanongo, Ngassa, Kiemba na Singano.
AZAM
Mwadini, Mao, salum, Atudo, Kakolaki,mwantika,
Blolou,Sure Boy,Mieno,Tchetche na Bocco.
0 COMMENTS:
Post a Comment