Huenda ikawa
kweli atarejea Chelsea lakini tayari Kocha Jose Mourinho amethibitisha
hatakuwepo Real Madrid msimu ujao.Mourinho maarufu kama amethibitisha ataondoka kutokana na kauli yake wakati akizungumza na Rais wa klabu ya Malaga.
“‘Mourinho ameniambia msimu ujao hatakuwa na mazungumzo yoyote na makocha kwa kuwa hatakuwepo Hispania,” rais huyo wa klabu inayotokea eneo la Canillas, Manuel Alvarez alipozungumza na gazeti la Punto Pelota.
“Kama Mourinho ataondoka mimi nilikuwa nafikiri itakuwa ni hasara kwa soka la Hispania kutokana na kazi yake, ninaamini Rais Florentino Perez atalishughulikia suala hilo.”
Inaelezwa Ufaransa ndiko zaidi Mourinho analenga kuelekea na hasa klabu za Monaco na Paris Saint Germain ingawa huenda nguvu ya tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich inaweza ikabadili mawazo yake.
Wakati Mourinho ameonyesha ataondoka zake, kumekuwa na taarifa kwamba kesho uongozi wa Real Madrid utakutana na kocha wake wa zamani Manuel Pellegrini aneyeinoa Malaga ili kumshawishi kurejea kuinoa baada ya Mourinho kuondoka.







0 COMMENTS:
Post a Comment