April 1, 2013





Chelsea imeituliza Man United kwa kuichapa bao 1-0 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA iliyochezwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, leo.

Bao la Chelsea lilipatikana katika dakika ya 49, mfungaji akiwa Mwafrika, Demba Ba ambaye aliunganisha pasi ya juu juu ya Juan Mata. Katika nusu fainali hiyo, Chelsea itawavaa jirani wa Man United, Manchester City.


Kwa ushindi huo, maana yake Chelsea imesonga hadi nusu fainali ya kombe la FA huku ikiondoa matumaini ya Man United kuendelea kuwemo katika kuwania kombe hilo lenye heshima nchini England.


Mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Manchester, timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2, hivyo kila upande ulitaka ushindi lakini wageni Chelsea walionekana kuwa bora zaidi leo.


Chelsea walipoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga kupitia Mata, Oscar, Ba na Hazzard wakati Man United walipata nafasi chache kupitia Chicharito na van Persie lakini hawakuzitumia au ziliokolewa.



  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic