Kiungo nyota wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’
amesema jezi namba 24 imekuw ana baraka kubwa kwake baada ya kufanikiwa kutwaa
ubingwa akiwa anaitumia.
Ukiachana na hivyo, Chuji amesema namba hiyo
imemsaidia kucheza vizuri katika msimu unaomalizika Mei 18 pamoja na kwamba
wengi waliamini haitawezekana.
“ Wakati nimerudi Yanga, wengi hawakuamini kama
nitacheza vizuri nikiwa natumia zaidi ya namba nne ambayo nilikuta anaivaa
Oscar Joshua.
“Lakini nikawaambia waniamini, sasa nimefanya
vizuri. Ninashukuru sana kwa kuwa ulikuwa msimu mzuri kwangu,” alisema Chuji.
“Naichukulia namba ishirini na nne kama moja ya
namba yenye bahati kwangu, nitaendelea kuitumia jezi hii.”
Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa ikiwa na mechi
mbili mkononi na mchango wa Chuji umekuwa mkubwa katika kikosi hicho cha
Jangwani.
Chuji amekuwa tegemeo katika kiungo cha ukabaji
maarufu kama duara la chini, lakini amekuwa akishirikiana vema na Haruna Niyonzima
raia wa Rwanda kuichezesha timu.







0 COMMENTS:
Post a Comment