![]() |
| Barthez.. |
Benchi la ufundi la Yanga, limechukua uamuzi wa
kuwapumzisha wachezaji wake wenye kadi mbili za njano kutocheza katika mechi ya
Jumatano dhidi ya Coastal Union.
Yanga inaivaa Coastal Union katika mechi yake hiyo
ya pili kabla ya kumaliza msimu na Kocha Mkuu, Ernie Brandts amepitisha suala
hilo.
Wachezaji wa Yanga wenye kadi mbili za njano ni Ally
Mustapha ‘Barthez’, David Luhende, Didier Kavumbagu, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon
Msuva na Hamis Kiiza.
![]() |
| Kiiza... |
Brandts amechukua uamuzi huo kutokana na kuhofia wanaweza kulambwa kadi nyingine ya njano halafu wakaikosa mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Simba.
Kutokana na uamuzi huo, huenda Yanga ikaonekana na
kikosi tofauti katika mechi hiyo ya Jumatano.
Haijajulikana kama anaweza kumtumia mchezaji mmoja
au wawili kati ya hao sita.
Lakini golini ataanza Said Mohammed ambaye amekuwa
hapati nafasi ya kutosha kutokana na umahiri wa Barthez langoni unaomfanya apate nafasi ya kuwania tuzo ya kipa bora wa msimu wa 2012-13.









0 COMMENTS:
Post a Comment