Ujumbe
wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) utakaowasili nchini keshokutwa
utaongozwa na Primo Corvaro.
Corvaro
ndiye anaonekana kukabidhiwa masuala yote ya migogoro na shirikisho hilo hasa
kwa upande wa bara la Afrika.
Imeelezwa
Corvaro ndiye amekuwa akishughulikia migogoro yote inayojitokeza katika nchi za
Afrika badala ya Ashford Mamelodi kama ilivyokuwa imezoeleka awali.
Hata
hivyo, kabla ya kukabidhiwa mikoba hiyo kutoka kwa bonge la mtu, Mamelodi,
Corvaro alilazimika kusoma taratibu mambo mengi kuhusiana na sola la Afrika
pamoja na siasa inavyochukua nafasi kubwa.
Imeelezwa
Mamelodi anatarajia kustaafu baada ya miaka michache, hivyo Corvaro ndiye
atachukua nafasi yake.
Ndiyo
maana katika masuala ya migogoro katika nchi kadhaa, Carvaro alilazimika
kusafiri na Mamelodi ili kujua mambo kadhaa yanavyokwenda.
Walikuwa
pamoja nchini Uganda, Februari mwaka jana kutatua mgogoro wa ligi ya soka
nchini humo ambao ulidumu kwa zaidi ya miezi miwili.
Mwaka
jana hiyohiyo, Corvaro alifanya kazi ya kubwa ya kumaliza suala la mgogoro
mwingine wa kisoka nchini Sierra Leone.
Corvaro
ndiye ataongoza timu itakayotua nchini Jumatatu, tayari kumaliza suala la
mgogoro wa uchaguzi mkuu wa TFF kwa kuwaona wagombea na kuwasilikiza, hasa wale
ambao wana madai ya kutotendewa haki na kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi au
vinginevyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment