Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwatangazia wadau wa mpira wa miguu
kuwa ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utawasili
nchini Jumatatu (Aprili 15 mwaka huu) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa
uchaguzi mkuu wa TFF.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka FIFA, ujumbe huo utaongozwa na Mkuu wa Idara ya
Uanachama ya FIFA, Primo Covarro na utafanya kazi kwa siku tatu kuanzia siku ya
ujio na kuondoka Aprili 18 mwaka huu.
Ukiwa
nchini, ujumbe huo utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao waliomba mashauri yao yaangaliwe
upya, wagombea ambao walikata rufani FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya
Rufani na Sekretarieti ya TFF.
Wajumbe
hao wangependa kukutana na waziri anayehusika na michezo, hivyo TFF imeiandikia
Wizara ikipendekeza kuwa ujumbe huo ukutane na Waziri na wakuu wengine wa
michezo Aprili 16 mwaka huu 2013 kabla ya kuanza kazi zao.
Wagombea
watakaosikilizwa na ujumbe huo wa FIFA ni:
1.
Farid Salim
Mbaraka Nahdi: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alienguliwa
na Kamati ya Uchaguzi na baadaye rufani yake kwa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi
ya TFF kutupwa na hali kadhalika ombi lake la kutaka shauri lake liangaliwe
upya, kukataliwa.
2.
Elliud Peter
Mvella: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na
Kamati ya Uchaguzi ya TFF na kukata rufani Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF
kabla ya maombi yake ya kutaka shauri lake kuangaliwa upya, kukataliwa.
3.
Mbasha Matutu:
Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya
Uchaguzi na kukata rufani ambayo pia ilitupwa kabla ya kuomba shauri lake
liangaliwe upya, ombi ambalo lilikataliwa.
4.
Hamad Yahya:
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi ambaye alipitishwa na Kamati ya
Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na kuondolewa. Aliomba shauri lake liangaliwe
upya, lakini Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ikatupa ombi lake.
5.
Jamal Emily
Malinzi: Mgombea wa nafasi ya urais wa TFF ambaye alipitishwa na Kamati ya
Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kuondolewa kwenye mchakato. Aliomba shauri
lake liangaliwe upya, lakini likakataliwa. Hata hivyo, alikuwa ameshakata
rufani FIFA.
6.
Michael Wambura:
Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF ambaye alikatwa na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF na rufani yake kukataliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya
TFF. Hakuomba shauri lake liangaliwe upya, lakini alikata rufani FIFA.
Shirikisho
linawaomba wote waliotajwa hapo juu kujiandaa kwa utetezi na maelezo ya kutosha
na kwamba barua za kuwaita zinafuata.
0 COMMENTS:
Post a Comment