April 13, 2013



 
Baba mzazi wa beki wa Yanga, Kelvin Yondani amesema anatamani kumuona mwanaye akikipiga nje ya nchi.

Patrick Yondani ambaye ni mwanasoka wa zamani, amesema anaamini Yondani ana uwezo wa kucheza soka la kulipwa katika klabu kubwa barani Ulaya ikiwezekana hata zile za Ulaya.


“Kweli Kelvin anajitahidi sana, naona anafanya vizuri hata katika mechi za kimataifa. Utaona ni zile ambazo zinajumuisha wachezaji mahiri kutoka Ulaya na kwingineko.

“Najua suala la kwenda Ulaya haliwezi kuwa sawa na kutoka Dar kuja Mwanza, lakini kiwango alichonacho ni vizuri akapata nafasi ya kucheza nje,” alisema.

Alisema anafurahishwa na mwenendo wake na anaamini akiendelea katika kiwango hicho atafanikiwa na kucheza nje.

Wakati akicheza soka, Patrick Yondani alikuwa mmoja wa washambuliaji wenye kasi.

Lakini mwanaye Yondani aliyejiunga na Yanga akitokea Simba msimu huu, ndiye amekuwa mhimili wa ulinzi kwa Yanga na timu ya soka ya taifa, Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic