Michuano ya Europa mechi ya marudiano hatua ya nusu fainali imekuwa na drama kibao baada ya timu mbili za England kutipwa nje.
England wenye mbwembwe nyingi wamejikuta wakiivusha timu moja tu kwenye nusu fainali ambayo ni Chelsea.
Rubin Kazan v Chelsea
Kwa England, Chelsea pekee wameonyesha ni vidume katika michuano ya Europa baada ya kusonga mbele hadi hatua ya nusu fainali.
Chelsea walikutana na kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Rubin Kazan wakiwa ugenini mjini Moscow, lakini matokeo ya kwanza ya 3-1 mjini London yakawaokoa.
Katika mechi hiyo iliyokuwa kali nay a kuvutia, Chelsea walishambulia mfululizo lakini makosa kadhaa katika safu yao ya ulinzi yaliwaangusha.
Fernando Torres alianza kazi mapema tu kwa kufunga bao katika dakika ya 5, lakini wenyeji wakajibu mapigo katika kipindi cha pili, dakika ya 51 Marcano akafunga na Moses akafunga la pili kwa Chelsea dakika ya 55.
Huku ikionekana kama Chelsea ingeweza kuibuka na ushindi ugenini, wenyeji walibadilika na kuanza kulisakama lango la wageni wao mfululizo.
Mabao ya harakaharaka katika dakika ya 62 kupitia Karadeniz na dakika ya 75 kupitia Natcho kwa mkwaju wa penalti yalibadilisha hali ya hewa na Chelsea wakalazimika kucheza kwa tahadhari kubwa.
Kikosi:
CHELSEA: Cech, Azpilicueta, Luiz, Terry, Ake, Ferreira, Benayoun (Oscar, 77), Ramires (Mikel, 60), Lampard (Ivanovic, 90), Moses, Torres
Sub haikutumika: Turnbull, Mata, Hazard, Marin.
Newcastle v Benfica
Newcastle ikiwa nyumbani, iliambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Benfica ambayo ilishinda bao 3-1 katika mechi ya kwanza ikiwa nyumbani kwao Ureno.
Kutokana na matokeo hayo, maana yake mabao kwa jumla yakawa 2-4 na Newcastle iliyokuwa imepania kulipa kisasi iliambulia patupu.
Spurs v Basel
Timu nyingine ya England, Tottenham ilijikuta ikilazimisha sare dhidi ya kwa mabao mawili ya Dempsey lakini katika mikwaju ya penalti ikalala.
Katika penalti tano tano, Spurs chini ya kocha Andre Villa Boas iliambulia moja tu hivyo kuwapa Basel ushindi we penalti 4-1.
Katika mechi hiyo iliyokuwa ya kibabe, wachezaji wanne wa Basel walilimwa kadi za njano sambamba na wanne wa Spurs ambayo mmoja wao, Vertonghen akalimwa nyekundu.
Lazio v Fenerbahce
Waitaliano
Lazio, wakiwa nyumbani walijikuta wakiiaga michuano hiyo dhidi ya Waturuki
wabishi timu ya Fenerbahce.
Pamoja na
kuwa ugenini, Fenerbahce walikomaa na kufanikiwa kulazimisha sare ya bao 1-1
baada ya Erkin kusawazisha katika dakika 73 wakati Lazio walianza katika dakika
ya 60 kupitia Lulic na walikuwa katika harakati ya kuongeza la pili.
Waturuki
hao wakiwa kwao katika mechi ya kwanza walishinda kwa mabao 2-0, hivyo matokeo
hayo ya mechi ya pili yamefanya matokeo ya jumla yake 1-3.
Fenerbahce
ina kikosi kinachoundwa na wachezaji kadhaa wazoefu wa michuanoi ya kimataifa
kama mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Dirk Kuyt na kiungo wa zamani wa
Chelsea, Meireles.
0 COMMENTS:
Post a Comment