April 12, 2013



Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema pamoja na mkanganyiko wa ratiba, anachotaka ni kuona wachezaji wake wanashinda ikibidi kwa idadi kubwa ya mabao.

Brandts raia wa Uholanzi, amesema wachezaji wake hawapaswi kuchanganywa na timu nyingine imeshinda mabao mangapi au inaendeleaje katika msimamo wa ligi.


“Tukianza kuangalia nani kafikisha pointi ngapi kwa kipindi hiki tutajichanganya, badala yake tunatakiwa kushinda na kuepusha mawazo tofauti.

“Kama tutashinda, tena kwa idadi kubwa ya mabao, basi hatuna sababu ya kuihofia timu nyingine tena,” alisema Brandts.

“Mechi yetu na Oljoro itakuwa muhimu ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha tunashinda mechi zote zilizobaki. Lazima tushinde mechi zote.”

Yanga ina pointi 49 kileleni na Jumamosi ina kazi ya kuivaa JKT Oljoro katika mechi muhimu kwao ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Yanga iko katika presha kubwa kwa kuwa wapinzani wao wakubwa kuwania ubingwa, Azam FC, leo jioni wameshinda kwa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon na kufikisha pointi 46.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic