April 12, 2013




Kipigo cha mabao 3-1 ilichokitia Taifa Stars katika mechi yake ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Morocco kimeisogeza Tanzania kwa nafasi tatu juu katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).


Taifa Stars chini ya Mdenish, Kim Poulsen iliyokuwa katika nafasi ya 119, imepanda chapchap hadi nafasi ya 116 huku baadhi ya nchi kama Korea Kaskazini ikipomoroka  kwa nafasi 13 hadi kufikia nafasi ya 115.

Tanzania imekuwa na mwendo mzuri kuanzia mechi za kirafiki, katika mechi zake tatu ilifanikiwa kushinda mbili za nyumbani na kufungwa moja tu. 

Mechi iliyopoteza ni dhidi ya Ethiopia ikiwa ugenini Addis Ababa, lakini ikawaonyesha kazi waliokuwa mabingwa Afrika Zambia kwa kuwachapa bao 1-0 kabla ya kuipa Cameroon kipigo kama hicho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic