Baada
ya Manchester United kutwaa taji la 20 la ubingwa wa Ligi Kuu England, beki
wake Patrice Evra ameherekea kwa staili ya aina yake inayoonekana kumdhihaki
mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez.
Evra
alionekana akishangilia akiwa na kipande cha mkono, dakika chache baada ya Man
United kuichapa Aston Villa na kubeba ubingwa.
Suarez
ndiye gumzo katika soka ukiachana na ubingwa huo wa Man United, ikiwa ni
kutokana na kitendo chake cha kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic.
Evra
na Suarez waliwahi kuingia katika mgogoro miezi kadhaa iliyopita baada ya Mruguay
huyo kutuhumiwa kumtolea Evra maneno ya kibaguzi.
Suarez
alikumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza mechi nane pamoja na kupigwa faini ya
noti za ‘malkia’.










0 COMMENTS:
Post a Comment