Kocha Mkuu
wa Kagera Sugar, Abdallah ‘King’ Kibadeni amesema makocha wazawa wanaweza
kuleta mabadiliko.
Kibadeni aliyewahi
kuwa mshambuliaji hatari wa Simba, amesema makocha wazawa wameonyesha wana
uwezo mkubwa katika msimu huu wa ligi.
Hivyo kuna
kila sababu ya viongozi wa klabu mbalimbali kuangalia suala la kuwapa nafasi.
“Angalia
Kagera, tunakwenda vizuri na Mtibwa Sugar na Coastal bado zina nafasi nzuri ya
kuendelea kupata pointi katika mechi za ligi.
“Lakini
Yanga imecheza na Mugambo na kupata wakati mgumu sana, ukilinganisha
anacholipwa kocha wa timu hiyo na wachezaji wao na wale wa Yanga kuna tofauti
kubwa.
“Kama
makocha wazawa wakipewa nafasi na kuaminiwa, wakalipwa vizuri zaidi huku
wakifanyiwa usajili mzuri, basi wanawea kufanya vizuri kuliko makocha wa
kigeni.
“Tuwaamini
kwa kuwa wanajua mengi kuhusiana na soka letu na wengi wapo wenye utaalamu
ingawa sina maana makocha wageni wasije nchini.”
Kibadeni ndiye
kocha mwenye rekodi nzuri zaidi kwa upande wa klabu kwa kuifikisha Simba katika
fainali ya Kombe la Caf mwala 1993 lakini ikapoteza mjini Dar es Salaam kwa
kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.







0 COMMENTS:
Post a Comment